Anda di halaman 1dari 6

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UCHUKUZI

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA


Simu ya mdomo: 255 22 2469706-8/2460735
Faksi: 255 22 2460735/2460700
Barua pepe: met@meteo.go.tz
Tovuti: www.meteo.go.tz

S.L.P. 3056
DAR ES SALAAM

Unapojibu tafadhali nakili:


Kumb. TMA/1622

31 Desemba, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


TATHMINI NA MWELEKEO WA MVUA NCHINI KWA KIPINDI CHA
JANUARI HADI MACHI, 2014
Taarifa hii inatoa tathmini ya mvua kwa msimu wa Oktoba hadi Disemba 27, 2013 na
mwelekeo wa mifumo ya hali ya hewa na mvua kwa kipindi cha miezi ya Januari hadi
Machi, 2014.
1.0

TATHMINI YA MVUA ZA VULI OKTOBA HADI DESEMBA 2013

Katika kipindi cha msimu wa mvua za Vuli Oktoba hadi Desemba 2013, maeneo mengi ya
nchi yamepata mvua chini ya wastani isipokuwa katika maeneo ya magharibi na yale ya
ukanda wa Ziwa Victoria ambayo yalipata mvua za wastani na maeneo machache ya Mikoa
ya Mara na Shinyanga yalipata mvua za juu ya wastani.
Vifuatavyo ni viwango vya mvua pamoja na wastani wa muda mrefu katika baadhi ya vituo
hivyo:
Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka:
Ukanda wa Ziwa Victoria:
Oktoba: Bukoba (64.7%), Mwanza (19.7%), Musoma (9.7%), Ukiriguru (36.9%) na
Shinyanga (38.1%); Novemba: Bukoba (76.0%), Mwanza (90.0%), Musoma (63.0%),
Ukiriguru (87.0%) na Shinyanga (60.0%); Disemba: Bukoba (1.7%), Mwanza (1.3%),
Musoma (199.1%), Ukiriguru (125.2%) na Shinyanga (229.4%).
Pwani ya Kaskazini pamoja naVisiwa vya Unguja na Pemba:
Oktoba: Zanzibar (53.4%), Amani (125.7%), Tanga (104.7%), Pemba (57.4%) na JNIA
(51.1%); Novemba: Zanzibar (64.0%), Amani (107.0%), Tanga (112.0%), Pemba (61.0%)
na JNIA (55.0%); Disemba: Zanzibar (43.7%), Amani (96.2%), Tanga (89.1%), Pemba
(97.4%) na JNIA (64.2%).
1

Nyanda za Juu Kaskazini-mashariki:


Oktoba: Arusha (4.1%), Lyamungo (40.0%), Kilimanjaro (0.0%) na Same (17.2%);
Novemba: Arusha (44.0%), Lyamungo (56.0%), Kilimanjaro (53.0%) na Same (96.0%);
Desemba: Arusha (51.0%), Lyamungo (56.0%), Kilimanjaro (87.6%) na Same (57.9%).
Maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua mara moja kwa mwaka:
Nyanda za Juu Kusini-magharibi:
Oktoba: Mahenge (105.2%) na Tukuyu (186.7%); Novemba: Mahenge (136.0%) na
Tukuyu (102.0%); Desemba: Mahenge (76.9%) na Tukuyu (0.0%).

Mikoa ya Magharibi:
Novemba: Tabora (44.0%), Kibondo (92.0%) na Kigoma (98.0%); Desemba: Tabora
(126.8%), Kibondo (34.97%) na Kigoma (137.3%).
Pwani ya Kusini:
Novemba: Kilwa (30.0%)
(83.2%).

na Mtwara (17.0%) ; Disemba: Kilwa (21.7%), Mtwara

Mikoa ya Kati:
Novemba: Singida (0.0%), Dodoma (0.0%) na Hombolo (0.0%); Disemba: Singida
(197.7%), Dodoma (60.3%) na Hombolo (28.4%).
Ruvuma:
Novemba: Songea (m%); Desemba: Songea (49.5%).

Kielelezo: Viwango vya mvua chini ya asilimia 75 ya wastani kwa kipindi kirefu hutafsiriwa
kama chini ya wastani, wakati viwango vya kati ya asilimia 75 hadi 125 hutafsiriwa kama
mvua za wastani na vile vya zaidi ya asilimia 125 hutafsiriwa kama juu ya wastani.
2.0 MWELEKEO WA MVUA ZA MSIMU WA JANUARI HADI MACHI 2014.
2.1: Utangulizi
Wataalam wa Mamlaka ya Hali ya Hewa walishirikiana na wataalam wengine katika
mkutano wa kutoa uchambuzi wa mwelekeo wa Mvua za Msimu wa Januari-Machi, 2014
katika nchi za kusini mwa Afrika (SADC) mnamo mwezi Agosti, 2013. Mwezi wa
Disemba, 2013 wataalam na wachambuzi wa masuala ya hali ya hewa na klimatolojia katika
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) walifanya uchambuzi wa mrejeo wa msimu .
Katika mkutano huo, tathimini ya kina katika mifumo ya hali ya hewa na athari zake kwa
msimu ujao wa mvua. Viashiria vikuu vilivyotumika ni pamoja na Hali ya joto la Bahari
katika maeneo ya Bahari ya Hindi, tropikali ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Atlantiki.
2

2.2: Mifumo ya hali ya hewa


Uchambuzi wa hali ya joto katika ukanda wa tropikali ya bahari ya Pasifiki, bahari ya
Atlantiki na Bahari ya Hindi pamoja na mwelekeo katika kipindi cha JanuariMachi 2014
unaonyesha hali ya joto la bahar kuwa la karibu na wastani. Vilevile joto la bahar la
wastani mashariki mwa bahar ya Hindi (Indonesia) na Magharibi mwa bahar ya Hindi
(Pwani ya Afrika ya mashariki) kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2014.
Kuimarika kwa mgandamizo mkubwa wa hewa katika maeneo ya Siberia kunatarajiwa
kusababisha upepo usio na unyevunyevu kutoka kaskazini-mashariki kuelekea maeneo
mengi ya nchi. Uwezekano wa kuongezeka kwa joto la bahar katika eneo la kusinimagharibi mwa bahar ya Hindi katika ya mwezi Januari hadi Machi 2014 kunatarajiwa
kusababisha uwezekano wa kutokea kwa vimbunga katika bahar ya Hindi.
Vilevile, kwa kipindi hiki kuwepo wa upepo kutoka magharibi unatarajiwa katika meneo
mengi ya nchi kutokana na kupunguwa kwa joto katika bahar ya Atlantiki.
2.3 Mwelekeo wa mvua kwa mwezi januari hadi machi, 2014
Kutokana na mifumo ya hali ya hewa kama ilivyoelezwa hapo juu, Mvua kwa kipindi cha
mwezi Januari hadi Machi, 2014 zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika
maeneo ya kusini mwa nchi na wastani hadi chini ya wastani katika maeneo ya kati na
magharibi mwa nchi.
(i)

Maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua (Pwani ya Kaskazini, Nyanda za Juu


Kaskazini-mashariki na ukanda wa ziwa Victoria):

Mvua za Vuli zinazoendelea katika maeneo yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka
(Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mwanza, Mara,
Geita, Shinyanga, Kagera na Simiyu) zinatarajiwa kuisha mwishoni mwa mwezi Disemba,
2013. Hata hivyo maeneo haya yanatarajiwa kupata mwendelezo wa mvua za nje ya msimu
(out of season rains) katika miezi ya Januari na Februari, 2014 katika maeneo ya kaskazini
hususan mwa mkoa wa Morogoro, kusini mwa mikoa ya Pwani na Manyara. Maeneo
mengine yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.
Utabiri wa mvua za masika katika maeneo haya utatolewa mwishoni mwa mwezi
Februari, 2014.
(ii)
Mvua za Msimu katika Maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua
Kipindi cha mvua za Msimu (Novemba hadi Aprili) zinaendelea na ni mahsusi kwa maeneo
yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (Kanda ya Magharibi, Kanda ya kati, Nyanda za
juu kusini magharibi, mikoa ya kusini na pwani ya kusini). Mvua zinazoendelea kunyesha
kwa kipindi cha Januari hadi Machi, 2014 zinatarajiwa kuwa kama ifuatavyo:Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Tabora, Rukwa, Katavi na kusini mwa Kigoma):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani
3

Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma):


Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.
Nyanda za juu Kusini Magharibi: (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa
mkoa wa Morogoro):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo ya mikoa ya Iringa,
Njombe, kusini mwa Morogoro na mashariki mwa mkoa wa Mbeya. Maeneo ya mwagharibi
mwa mkoa wa Mbeya yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani.
Kanda ya kusini na Pwani ya kusini (Mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi):
Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu wastani isipokuwa kaskazini mwa mkoa wa
Lindi ambapo mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani.

Uwezekano wa kupata
mvua zilizo nje ya
msimu kwa mwezi
Januari na Februari
2014

MUHIMU: Kuwepo kwa vimbunga katika bahari ya Hindi kunaweza kusababisha


mabadiliko ya mifumo ya hali ya hewa. Mamlaka ya Hali ya Hewa itaendelea kufuatilia
mifumo na mienendo ya hali ya hewa na kutoa taarifa na ushauri kila itakapobidi.

Taarifa katika jedwali linaonyesha uwezekano (probability) kwa mfano maeneo ya kusini
uwezekano wa kupata mvua za juu ya wastani ni asilimia arobaini 40%, mvua za wastani
35% na mvua za chini ya wastani 25%.

3.0 ATHARI NA USHAURI (Yonah, Waniha, Mlonganile, Bibie)


3.1: Kilimo na usalama wa chakula
Upungufu wa unyevunyevu kwenye udongo unatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata
mvua mara mbili kwa mwaka. Maeneo hayo ni mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu,
Shinyanga, Manyara, Kilimanjaro na maeneo ya Arusha, Dar es Salaam, Tanga, mkoa wa
Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba. Hali hii inatarajia kusaidia uvunaji na uhifadhi wa
mazao, na inaweza kuathiri mazao ya Vuli yaliyopandwa kwa kuchelewa.
Maeneo yanayopata mvua mara moja kwa mwaka (mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe,
Ruvuma, Lindi, Mtwara, Katavi, kusini mwa mkoa wa Tabora, Singida, Dodoma na
Morogoro) yanatarajiwa kupata unyevuyevu wa kutosha kwenye udongo. Wakulima katika
mikoa hii wanashauriwa kuendelea na shughuli za kilimo kama kawaida. Hata hivyo, mvua
za juu ya wastani zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mtwara, Lindi,
Ruvuma, Kusini mwa mkoa wa Morogoro, na Njombe yanatarajia kusababisha
unyevunyevu mwingi kupita kiasi kwenye udongo na unaweza kuathiri ukuaji wa mazao na
utunzaji wa mashamba. Wakulima wanashauriwa kutafuta ushauri wa kitaalam kutoka kwa
Afisa Ugani.
3.2: Malisho na maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori
Hali ya malisho na maji kwa ajili ya mifugo na wanyamapori inatarajiwa kuimarika katika
maeneo mengi yanayopata mvua mara moja kwa mwaka. Hata hivyo, maeneo mengi
yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka hayatakuwa na ongezeko la maji na malisho na
hivyo wafugaji wanashauriwa kutumia maji kwa uangalifu.
3.3: Nishati na maji
Kiwango cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka hususan katika
maeneo yanatarajiwa kuwa na mvua za wastani na juu ya wastani. Hata hivyo, maeneo
mengi yanayopata mvua mara mbili kwa mwaka hayatarajiwi kuwa na ongezeko. Izingatiwe
kuwa vina vya maji havikuongezeka sana kutokana na mvua za Vuli kuwa hafifu, hivyo
matumizi ya maji kwa ajili yafanyike kwa uangalifu.

3.4: Mamlaka za miji


Vipindi vya mvua kubwa vinaweza kujitokeza katika maeneo yanayotarajiwa kupata mvua
chini ya wastani. Hivyo mamlaka za manispaa na miji zinashauriwa kusafisha mitalo ya
maji taka ili kuepusha kutuama kwa maji na kusababisha mafuriko.
5

3.5: Sekta ya afya


Kuna uwezekano wa kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama vile malaria na kipindupindu
katika maeneo mbalimbali nchini. Hivyo hatua za tahadhari zichukuliwe
3.6: Menejimenti ya Maafa
Kamati za maafa kwenye vituo vya kitaifa vinavyoshughulikia maafa zinashauriwa
kuchukua hatua muafaka zitakazokabiliana na athari zitokanazo na utabiri huu. Maeneo
yanayotarajiwa kupata mvua juu ya wastani yanauwezekano wa kupata mafuriko,
mmomonyoko wa ardhi na uharibifu wa miundombinu. Hata hivyo maeneo yanayopata
mvua chini ya wastani yanatarajiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata uhaba wa
chakula.
3.7: Vyombo vya habari
Vyombo vyote vya habari vinasisitizwa kutafuta, kupata na kusambaza taarifa za hali ya
hewa zinazotolewa na Mamlaka. Watumiaji nao wanashauriwa kufuatilia taarifa hizo
kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kuzitumia kwa ukamilifu.
Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania itaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya hali
ya hewa na kutoa taarifa za mwelekeo wa mvua nchini.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

Anda mungkin juga menyukai