Anda di halaman 1dari 32

Aqiydah Ya Maimaam Wa

Hadiyth


Imaam Abu Bakr Ismaa`iyliy
(277-371)

Mfasiri:
Abu Bakr al-Khatwiyb al-Atrush

Imepitiwa Na:
Abu Abdillaah Muhammad Baawazir
1
www.alhidaaya.com

YALIYOMO
Msingi Wa Itikadi Ya Ahlul-Hadiyth .............................................................................. 4
Kauli Kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake ............................................................... 4
Baadhi Ya Vipimo Hususan Vya Ubwana Wake .......................................................... 5
Kuthibitisha Asmaauhu Al-Husnaa (Majina Mazuri) Ya Allaah Na Swifaatuhul
`Ulaa (Sifa Zake Kuu) ......................................................................................................... 5
Kuthibitisha Sifa Ya Mikono ............................................................................................ 5
Kauli Yao Kuhusu Sifa Ya Uso Wake, Kusikia Kwake, Kuona, Elimu, Uwezo Na
Maneno Yake ........................................................................................................................ 6
Kuthibitisha Mashiy-ah (Matakwa) Ya Allaah.............................................................. 9
Elimu Ya Allaah.................................................................................................................. 10
Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah........................................................................................ 10
Matendo Ya Waja Yameumbwa Na Allaah .................................................................. 10
Kheri Na Shari Inatoka Kwa Allaah .............................................................................. 13
Kushuka (Kwa Allaah) Katika As-Samaa' Ad-Dunyaa (Mbingu Ya Dunia)......... 13
Waumini Kumuona Mola Wao Aakhirah ..................................................................... 14
Ukweli Wa Iymaan ............................................................................................................ 15
Kauli Yao Kuhusu Yule Mwenye Kufanya Madhambi Makubwa ......................... 15
Hukmu Ya Mwenye Kuacha Swalah Kwa Makusudi................................................ 16
Kauli Za Wanachuoni Kuhusu Tofauti Kati Ya Uislamu Na Iymaan ..................... 17
Shafaaah (maombezi), Hawdh (Kisima cha Mtume), Maaad (Qiyaamah) Na
Hesabu.................................................................................................................................. 19
Kutoa Ushuhuda Mmoja Katika Watu Wa Tawhiyd Kwa Pepo Au Moto............. 19
2
www.alhidaaya.com

Adhabu Ya kaburi.............................................................................................................. 20
Maswali Ya Munkar Na Nakiyr ...................................................................................... 22
Kuacha Ugomvi Na Majadiliano Katika Dini.............................................................. 22
Ukhalifa (Uongozi) Wa Al-Khulafaa' Ar-Raashiduwn............................................... 23
Ubora Baina Ya Maswahaba ............................................................................................ 23
Kauli Yao Juu Ya wale wanaowachukia Maswahaba................................................. 24
Swalah Ya Ijumaa Nyuma Ya Kila Imaam Muislamu, Sawa Wakiwa Wema Au
Waovu................................................................................................................................... 27
Jihaad Pamoja Na Viongozi Hata Kama Waovu.......................................................... 28
Nchi Ya Kiislamu ............................................................................................................... 28
Matendo Ya Waja Hayawajibishi Kuingia Peponi, Bali Ni Kutokana Na Fadhila
Za Allaah.............................................................................................................................. 28
Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye Kuruzuku Daima)............................................ 29
Allaah Ndiye Kaumba Mashayatwiyn Na Wasiwasi Wao ........................................ 30
Uchawi Na wachawi .......................................................................................................... 30
Kujitenga Na Bidah .......................................................................................................... 30
Kujifunza Elimu................................................................................................................. 31
Kujizuia [Kuwaongelea Vibaya] Maswahaba ............................................................. 31
Kushikamana Na Jamaaah .............................................................................................. 31
Uwajibu Wa Kushikamana Na Madh-hab Ya Ahlul-Hadiyth, Firqatun-Naajiyah
(Kipote Kitakachookoka) ................................................................................................. 31

3
www.alhidaaya.com

Ibn Qudaamah kasema: Ametujulisha ash-Shariyf Abul-Abbaas Masuud bin


Abdil-Waaahid bin Matwar al-Haashimiy kasilimulia na kusema: Haafidh AbulAlaa Saiyd bin Yasaar al-Harawiy katusimulia: Abul-Hasan Aliy bin
Muhammad al-Jurjaaniy katusimulia: Abul-Qaasim Hamzah bin Yuusuf asSahmiy katusimulia: Abu Bakr Ahmad bin Ibraahiym Ismaaiyliy kasema:

Msingi Wa Itikadi Ya Ahlul-Hadiyth


Jua Allaah Atubariki sisi na ninyi ya kwamba Madhehebu ya AhlulHadiyth, Ahlus-Sunnah wal-Jamaaah imejengwa
chini
ya
msingi
wa
kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake na kukubali yale
yaliyokuja katika kitabu cha Allaah (Taala), na yale yaliothibiti katika
riwaya sahihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa
sallam).
Hakuna kuyafanyia ta-awiyl yale yaliosimuliwa kutoka Kwake na wala hakuna
nafasi ya kuyakataa. Yote haya kwa kuwa wameamrishwa kufuata Kitabu
na Sunnah. Wanaamini kuwa yote yana uongofu na wanashuhudia kwamba
Mtume wao (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) anaongoza katika Njia
iliyonyooka wakati huohuo wanachukua tahadhari kwenda kinyume naye
kutokana na fitnah na adhabu iumizayo isije kuwapata.

Kauli Kuhusu Majina ya Allaah na Sifa Zake


Na wanaitakidi kwamba Allaah (Subhaanahu wa Taala) Anaombwa kwa
Majina Yake mazuri ambayo Kajiita Kwayo Mwenyewe, na Sifa Zake ambazo
Kajisifia nazo Mwenyewe na kwa Majina na Sifa ambazo Mtume Wake (Swalla
Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) kamsifu au kumueleza Kwazo. Alimuumba
4
www.alhidaaya.com

Aadam (Alayhis Salaam) kwa Mkono Wake. Mikono Yake ni mikunjufu


na Huitumia Apendavyo, bila Kayf (kutaka kujua vipi au ikoje). Hakika Allaah
(Taala) istawaa juu ya Arshi Yake na Hakueleza istiwaa (Kuwa Kwake juu ya
Arsh) Yake ni vipi na kukoje!

Baadhi Ya Vipimo Hususan Vya Ubwana Wake


Yeye ndiye Mmiliki wa uumbaji Wake. Hakuumba kwa sababu Anafanya lolote
Atakalo
na
Anahukumu
kama
Apendavyo.
Haulizwi
kwa
Alifanyalo, lakini viumbe wao wataulizwa kwa yale waliyoyatenda.

Kuthibitisha Asmaauhu Al-Husnaa (Majina Mazuri) Ya Allaah Na Swifaatuhul


`Ulaa (Sifa Zake Kuu)
Yeye huitwa (huombwa) kwa Majina Yake, na Yeye husifiwa kwa Sifa Zake
Alizojisifia nazo Mwenyewe na alizosifiwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu
alayhi wa aalihi wa sallam). Hakuna kitu chochote katika ardhi wala mbinguni
kisichowezekana Kwake. Hasifiki kwa kasoro au mapungufu, hakika Allaah
(Taala) yuko mbali na hayo.

Kuthibitisha Sifa Ya Mikono


Alipomuumba Aadam (Alayhis Salaam) Alimuumba kwa mikono Yake. Mikono
Yake ni mikunjufu na Anaitumia Atakavyo, bila ya kuwa na haja ya kuitakidi
5
www.alhidaaya.com

ikoje mikono Yake, kwa kuwa Kitabu cha Allaah (Taala) hakikuzungumzia ni
namna gani ilivyo.
Wala isiitakidike (kwa mtu) ya kwamba Ana viungo, urefu, upana, unene,
wembamba au mfano wa sifa kama hizo ambazo ni mfano wa sifa za viumbe
Wake. Na Yeye (Tabaaraka wa Taala) hakuna kitu mfano Wake, umetukuka
wajihi wa Bwana wetu, Subhaanahu wa Taala.
Hawaamini kama Mu`tazilah wasemavyo kuwa Majina ya Allaah (Azza wa Jalla)
yameumbwa, kama pia wanavyoamini Khawaarij na makundi mengine katika
makundi ya watu wa matamanio (Ahlul-Bidah).

Kauli

Yao

Kuhusu Sifa Ya Uso Wake, Kusikia


Elimu, Uwezo Na Maneno Yake

Kwake,

Kuona,

Wao wanathibitisha Uso Wake, Kusikia Kwake, Kuona, Elimu, Uwezo, Nguvu,
Maneno, lakini si kwa njia ya watu wapotofu kama Mu`tazilah na wengine
wanavyosema, isipokuwa ni kama Yeye (Taala) Alivyosema:

Na Utabakia Uso wa Mola wako Mwenye utukufu na ukarimu [Ar-Rahmaan


55: 27].

6
www.alhidaaya.com

Na Anasema:

Ameyateremsha kwa kujua Kwake [An-Nisaa 4: 166].

Na Anasema:

Wala wao hawajui chochote katika vilio katika (elimu) ujuzi Wake, ila kwa
Atakalo Mwenyewe. [Al-Baqarah 2: 255].

Vilevile Anasema:

Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Allaah. Kwake Yeye
hupanda neno zuri, na amali njema Yeye Huitukuza. Na wanaopanga vitimbi
vya maovu watapata adhabu kali. Na vitimbi vya haovitaondokea patupu.
[Faatwir 35: 10].

7
www.alhidaaya.com

Pia kasema:

Kwani wao hawakuona kwamba Allaah Aliyewaumba ni Mwenye nguvu


kushinda wao? [Fusswilat 41: 15]

Pia kasema:

Hakika Allaah ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. [AdhDhaariyat 51: 58].

Yeye (Subhaanahu wa Taala) Ana Elimu, Nguvu, Usikivu, Uoni, na Maneno,


kama Yeye (Subhaanahu wa Taala) Anavyosema:

Ili ulelewe machoni Mwangu. [Twaahaa 20: 39].





8
www.alhidaaya.com

Na unda jahazi mbele ya macho yetu na kwa mujibu wa ufunuo wetu. [Huwd
11: 37].

Na ikiwa mmojawapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi


apate kusikia maneno ya Allaah. [At-Tawbah 9: 06].

Na Allaah Alizungumza na Muwsaa kwa maneno. [An-Nisaa 4: 164].

Hakika amri Yake Anapotaka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa. [Yaasiyn
36: 82].

Kuthibitisha Mashiy-ah (Matakwa) Ya Allaah


Wanasema kama wasemavyo Waislamu wote:
"Kile Apendacho Alllaah hutokea, na kila Asichopenda hakitokei.
Kama Alivyosema Allaah (Taala):
9
www.alhidaaya.com

Wala nyinyi hamtotaka isipokuwa Atake Allaah Mola wa walimwengu wote.


[At-Takwiyr 81: 29].

Elimu Ya Allaah
Wanasema kwamba hakuna njia kwa mtu yeyote ya kuweza kuzidi Elimu ya
Allaah, na wala hakuna tendo la mtu au matakwa yawezayo kushinda Matakwa
ya Allaah, wala kubadilisha Elimu ya Allaah, kwa kuwa Yeye ni Mwenye ujuzi
[elimu] na hatumbukii kwenye ujinga wala kusahau. Yeye ni mwenye Uwezo na
ambao hakuna awezaye kuushinda.

Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah


Wanasema
kwamba
Qur-aan
ni
Maneno
ya
Allaah
na
hayakuumbwa. Hayakuumbwa jinsi msomaji atavyoyasoma na kuyatamka, na
yamehifadhiwa kwenye vifua, yakisomwa kwa ndimi, yameandikwa kwenye
msahafu. Yule atayesema kuwa utamshi wa Qur-aan umeumbwa na akikusudia
Qur-aan, atakuwa amesema kwamba Qur-aan imeumbwa.

Matendo Ya Waja Yameumbwa Na Allaah


Wanasema kwamba hakuna Muumba halisi isipokuwa Allaah (Azza wa Jalla).
Mafanikio ya waja wote yameumbwa na Allaah. Allaah Humuongoza Amtakaye
10
www.alhidaaya.com

na Humpoteza Amtakaye. Hahojiwi kwa yule ambaye Allaah (Azza wa Jalla)


kampoteza, kama Asemavyo Allaah (Taala):

Sema: Basi Allaah ndiye Mwenye hoja yakukata. Na kama Angelipenda Aangeli
kuhidini nyote. [Al-Anaam 6: 149].

Pia Kasema:

Kama Alivyokuumbeni mwanzo ndivyo mtavyorudi [Al-Aaraaf 7: 29].


Pia Kasema:

Hali ya kuwa kundi moja Amelihidi, na kundi jingine limethibitikiwa na


upotofu. [Al-Aaraaf 07 : 30 ].

Pia Kasema:

11
www.alhidaaya.com

Na Tumeiumbia Jahannam majini wengi na watu. [Al-Aaaraf 7: 179].

Pia Kasema:

Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa
katika Kitabu kabla Hatujauumba. [Al-Hadiyd 57: 22].
Nabra-ahaa maana yake ni kuumba bila ya utata wowote katika lugha.

Anasema kuhusu watu wa Peponi:


AlhamduliLlaah! Kuhimidiwa ni kwa Allaah, ambaye Ametuhidi kufikia haya.
Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingelikuwa Allaah Hakutuhidi. [AlAaraaf 7 : 43].

Pia Kasema:






12
www.alhidaaya.com

Allaah Angelitaka bila ya shaka Angeliwaongoa watu wote [Ar-Ra`d 13: 31].
Pia Kasema:









Na Angelitaka Mola wako Angewafanya watu wote wakawa ummah mmoja.
Lakini hawaachi kukhitalifiana [Huwd 11: 118].

Pia Kasema:



Isipokuwa wale ambao Mola wako Amewarehemu [Huwd 11: 119].

Kheri Na Shari Inatoka Kwa Allaah


Wanasema kwamba kheri na shari, mazuri na mabaya ni kutokana na matakwa
ya Allaah (Azza wa Jalla). Ameyaacha yatokee na kuyakadiria tangu mwanzo
(kwa hekima Yake), na hayamiliki madhara wala natija isipokuwa Apendavyo
Allaah. Wao ni mafukara mbele ya Allaah (Azza wa Jalla) Ambaye kamwe hawi
na haja yao.

Kushuka (Kwa Allaah) Katika As-Samaa' Ad-Dunyaa (Mbingu Ya Dunia)


Yeye (Azza wa Jalla) Hushuka katika mbingu ya dunia kutokana na mapokezi
13
www.alhidaaya.com

sahihi yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa


sallam) bila ya itikadi ya Kayf (kuuliza Anashukaje).

Waumini Kumuona Mola Wao Aakhirah


Wanasema waja wamchao Allaah watamuona Allaah (Azza wa Jalla) Siku ya
Qiyaamah, si Duniani. Na wale ambao Allaah Amewavika katika mavazi Yake
Atakuja kuwajaalia hilo siku ya Qiyaamah, kama Alivyosema Allaah:






Zipo nyuso siku hiyo zitakazongara, Zinamwangalia Mola wao. [Al-Qiyaamah
75: 22-23].
Yeye (Subhaanahu wa Taala) Anasema kuhusu Makafiri:

Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa (kumuona Allaah). [AlMutwaffifiyn 83: 15].

Ingekuwa Waumini na makafiri wote wasingelimuona (Allaah), wangezuiliwa


kumuona. Na hili bila ya itikadi ya kumpigia mithali ya mwili Allaah na bila ya
kumfanyia mipaka. Bali watamuona Allaah (Azza wa Jall) kwa macho yao kwa
njia Atakayo, bila ya Kayf (kuuliza namna ipi ).
14
www.alhidaaya.com

Ukweli Wa Iymaan
Wanasema kuwa Iymaan ni kauli na matendo na maarifa. Inaongezeka kwa utiifu
na inapungua kwa maasi. Yule anayetii sana Iymaan yake inazidi kuliko yule
mwenye utiifu mdogo.

Kauli Yao Kuhusu Yule Mwenye Kufanya Madhambi Makubwa


Wanasema ikiwa mmoja katika watu wa Tawhiyd ambaye anaswali kuelekea
Qiblah cha Waislamu akifanya dhambi, au madhambi; makubwa, au madogo
pamoja na kuwa ana itikadi ya Tawhiyd kwa Allaah huku akikubali yale ambayo
Allaah kamuwajibishia juu yake, hahukumiwi kuwa kafiri kwa sababu ya
kufanya hayo [madhambi]. Wanamtarajia [mtu huyo] msamaha. Anasema
(Subhaanahu wa Taala):

Na Husamehe mengine yasiyokuwa hayo (Shirk) kwa amtakaye. [An-Nisaa 4:


48].

15
www.alhidaaya.com

Hukmu Ya Mwenye Kuacha Swalah Kwa Makusudi


Wametofautiana juu ya mtu ambaye kaacha swalah za faradhi kwa makusudi na
bila ya dharurah mpaka muda wake ukatoweka. Baadhi yao wamewakufurisha
kutokana na riwaya zilizopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu alayhi
wa sallam):

Baina ya mja na baina ya Kufru [ukafiri] ni [mtu] kuacha Swalah [Swahiyh atTarghiyb Wat-Tarhiyb, Hadiyth 563. Kutoka kwa Ibn Maajah].
na:

Yeyote mwenye kuacha Swalah basi amekufuru [Swahiyh at-Targhiyb WatTarhiyb, Hadiyth 575].
na:

16
www.alhidaaya.com

Yeyote yule mwenye kuacha Swalah, sina ulinzi wa Allaah kutoka kwake
[Swahiyh at-Targhiyb Wat-Tarhiyb, Hadiyth 569 kutoka kwenye ukusanyaji wa
atw-Twabaraaniy].

Na kundi lingine wamelifasiri (kinyume kwa kukataa) hili. wanasema ni


mpaka akatae uwajibu wake. Kama alivyosema Yuwsuf (Alayhis-Salaam):

Hakika mimi nimeacha mila ya watu wasiomuamini Allaah [Yuwsuf 12: 37].

Hivyo wameacha [kuamini] ndio Kufru.

Kauli Za Wanachuoni Kuhusu Tofauti Kati Ya Uislamu Na Iymaan


Baadhi yao wanasema kuwa Iymaan ni kauli na matendo, na Uislamu ni kufanya
yale matendo ambayo mtu kawajibishiwa kuyafanya. Hivyo kukasemwa kwamba
Waumini na Waislamu ni maneno mamoja yenye maana tofauti; kukitajwa [neno]
moja hakukusudiwi lingine. Lakini ikiwa kutatajwa [neno] moja, huingia yote
mawili. Anasema Allaah (Taala):

17
www.alhidaaya.com

Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitokubaliwa kwake. [Al-Imraan 3:


85].
Hivyo mtu akichagua Iymaan nyingine [dini kinyume na Uislamu], hatokubaliwa.
Na Akasema tena Allaah (Taala):

Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu... [AdhDhaariyaat 51: 36-7].
Wengine wakasema kuwa Uislamu na Iymaan ni [neno] moja. Kama Alivyosema
Allaah (Azza wa Jalla):

Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walioamini. Lakini hatukupata humo ila
nyumba moja tu yenye Waislamu! [Adh-Dhaariyaat 51: 36-37].

Akasema tena:

Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni:


Tumesilimu. Kwani Iymaan haijaingia katika nyoyo zenu. [Al-Hujuraat 49: 14].
18
www.alhidaaya.com

Na Akasema tena:

Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu.


Bali Allaah ndiye aliyekufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Iymaan [AlHujuraat 49: 17].
Na hizi ni dalili za wale wanaosema kuwa yote ni mamoja.

Shafaaah (maombezi), Hawdh (Kisima cha Mtume), Maaad (Qiyaamah) Na


Hesabu
Wanasema Allaah Atawatoa Motoni watu wa Tawhiyd (Ahlul-Tawhiyd) baada ya
uombezi wa waombezi. Na kwamba Shafaaah (maombezi) ni kweli. Hawdh ni
kweli. Qiyaamah ni kweli na Hesabu ni kweli.

Kutoa Ushuhuda Mmoja Katika Watu Wa Tawhiyd Kwa Pepo Au Moto


Hawamthibitishii yeyote katika watu wa Tawhiyd kwamba ni katika watu wa
Peponi au Motoni, kwa sababu elimu hiyo imefichikana kwao na hawajui ni
katika hali ipi mtu kafa kwayo; Iymaan au Kufr? Lakini wanasema ikiwa mtu
amekufa katika Uislamu bila ya kuwa na madhambi makubwa, hawaa na
matendo machafu basi [huyo] ni katika watu Peponi. Kutokana na kauli Yake
(Subhaanahu wa Taala):

19
www.alhidaaya.com

Hakika walioamini na wakatenda mema,... [Al-Bayyinah 98: 7-8].


Wala (Allaah) Hajasema wakafanya madhambi.

.... hao ndio bora wa viumbe Malipo yao kwa Mola wao ni Bustani za daima
(Peponi). [Al-Bayyinah 98: 7-8].
Pia yule ambaye Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) kamshuhudia Pepo
ambayo yamepokewa katika Hadiyth sahihi, nao (Ahlul-Hadiyth) humshuhudia
[mtu huyo] kwa kumfuata Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam)
na kuthibitisha maneno yake.

Adhabu Ya kaburi

Wanasema kuwa adhabu ya kaburi ni kweli. Allaah Atamuadhibu yule


anayestahiki kuadhibiwa Akitaka, na Humsamehe Akitaka. Allaah (Taala)
Anasema:

20
www.alhidaaya.com

Wanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itakapofika Saa ya Qiyaamah


patasemwa: Waingizeni watu wa Firawn katika adhabu kali kabisa. [Ghaafir
40: 46].

Hivyo imethibitishwa ya kuwa maadamu masiku yangali ya maisha haya ya


dunia - mchana na usiku - Allaah Atawaadhibu usiku na mchana mpaka siku
Qiyaamah kitapokuja watapewa adhabu kali bila ya kupunguziwa kutokana na
waliyoyafanya duniani. Allaah Anasema:


Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye
dhiki, [Twaahaa 20: 124].
Maana yake ni kabla ya kuisha maisha ya duniani, kutokana na kauli Yake
(Subhaanahu wa Taala):

... na Siku ya Qiyaamah tutamfufua hali ya kuwa kipofu. [Twaahaa 20: 124].

Yaani (maana yake) kwamba maisha ya dhiki huja kabla ya siku ya Qiyaamah.
Kutokana na uzoefu wetu wetu Mayahudi, Wakristo na Washirikina wana maisha
ya raha na ustawi. Ni juu yetu kujua ya kwamba dhiki hii haina chochote
kuhusiana na hali ya riziki kwa kuwa (twajua sote kwamba) washirikina wako
katika hali nzuri kuhusiana na riziki hapa duniani. Kikusudiwacho ni maisha
baada ya kifo na kabla ya Qiyaamah.

21
www.alhidaaya.com

Maswali Ya Munkar Na Nakiyr


Wanaamini pia maswali ya Munkar na Nakiyr kutokana na habari zilizothibiti
sahihi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) na kauli
ya Allaah (Subhaanahu wa Taala):

Allaah Huwathibitisha imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha
ya dunia na katika Aakhirah. Na Allaah Huwaacha kupotea hao wenye
kudhulumu. Na Allaah hufanya Apendavyo. [Ibraahiym 14 : 27].
Na kufuata haya kwa tafsiri iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu
alayhi wa sallam).

Kuacha Ugomvi Na Majadiliano Katika Dini


Wanaonelea kuacha ugomvi na mabishano juu ya masuala ya Qur-aan na
mengineyo, kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Taala):

Hawazibishii Ishara za Allaah ila ambao wamekufuru. [Ghaafir 40: 04].

22
www.alhidaaya.com

Yaani wanayajadili (watu kwa wengine) na kuyasemea uongo, na Allaah Anajua


zaidi.

Ukhalifa (Uongozi) Wa Al-Khulafaa' Ar-Raashiduwn

Wanathibitisha ukhalifa wa Abu Bakr (Radhiya Allaahu anhu) baada ya Mtume


wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) kwa sababu Maswahaba
walimteuwa; halafu ukhalifa wa 'Umar (Radhiya Allaahu anhu) baada ya Abu
Bakr kumteua kama Khaliyfah; halafu ukhalifa wa 'Uthmaan (Radhiya Allaahu
anhu) baada ya makubaliano ya mashauri ya Waislamu yaliyofanyika kwa
utaratibu wa Umar. Halafu ukhalifa wa Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu
anhu) chini ya msingi wa ba`iyah na ahadi iliyotolewa na wale ambao
walioshuhudia vita vya Badr, kama Ammaar bin Yaasir, na Sahl bin Hunayf, na
Maswahaba wengine waliyowafuata katika hilo kutokana na haki na fadhila
zilizotajwa (za Aliy).

Ubora Baina Ya Maswahaba


Wanasema Maswahaba (Radhiya Allaahu anhum) ndio watu bora kutokana na
Kauli Yake Allaah:

Kwa hakika Allaah Amewapa radhi Waumini walipofungamana nawe chini ya


mti. [Al-Fath 48: 18].
23
www.alhidaaya.com

Pia Kasema:

Na wale waliotangulia, wa kwanza, katika Muhaajiruwn na Answaar, na


waliowafuata kwa wema, Allaah Ameridhika nao, na wao wameridhika naye;...
[At-Tawbah 9: 100].

Yule ambaye Kathibitisha Allaah radhi Zake juu yake, hatokuja kupatwa baada ya
hilo na kitu kitachosababisha kupatwa na hasira za Allaah (Azza wa Jalla). Wale
wanaowachukia na kuwaponda hawapewi uzito wowote na huchukuliwa si
lolote wala chochote.

Kauli Yao Juu Ya wale wanaowachukia Maswahaba


Yule mwenye kuchukia kutokana na nafasi zao kwa Allaah, hakuna hofu kubwa
kwa kitu kama hofu kubwa iliyoko (ahofiwayo) juu yake. Kutokana na kauli Yake
Allaah (Subhaanahu wa Taala):

24
www.alhidaaya.com

Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya


makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama nakusujudu
wakitafuta fadhila na radhi za Allaah. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari
ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Tawraat. Na mfano wao katika Injiyl ni
kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene,
ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili
kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Allaah Amewaahidi walioamini na
wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa. [Al-Fat-h 48: 29].
Hivyo Kasema ya kwamba Kawafanya (Maswahaba) kuwa wakali mbele ya
Makafiri.
Wanasema kuhusu ukhalifa wao ni sahihi, kutokana na kauli Yake Allaah
(Subhaanahu wa Taala):

Allaah Amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema,...


[An-Nuwr 24: 55].

Kwa kauli Yake miongoni mwenu ni dalili ya kwamba ni wale ambao


walikuwa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam) kunako dini
yake. Akaendelea kusema:

25
www.alhidaaya.com

...Atawafanya Makhalifa (Waongozi) katika ardhi kama alivyowafanya


makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini Atawasimamishia Dini yao
Aliyowapendelea, na Atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe
wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. [An-Nuwr 24: 55].

Allaah kaipa Dini uimara kupitia nguvu za Abu Bakr, 'Umar na `Uthmaan; Allaah
Kawapa ahadi ya usalama, walipigana vita na kushinda wao na hawakushindwa,
na walitisha maadui zao na hawakuwahi kutishwa na maadui zao.

Allaah pia Kasema kwa wale waliobaki nyuma na Mtume katika vita ya kwamba
Atawapambanua katika kupigana kwa kauli Yake:

Basi Allaah Akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na


wakakutaka idhini ya kutoka - sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala
hamtopigana na adui pamoja nami. Nyinyi mliridhia kukaa nyuma mara ya
kwanza, basi kaeni pamoja na hao watakaobakia nyuma. [At-Tawbah 9: 83].

Hivyo waliokuwa hai wakati wa Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa sallam)


walimuomba ruhusa ya kwenda nje kwenye vita dhidi ya adui, lakini (Mtume)
hakuwapa ruhusa. Ndipo Allaah (Subhaanahu wa Taala) Alipoteremsha (aayah)
zifuatazo:

26
www.alhidaaya.com

Waliobaki nyuma watasema: Mtakapokwenda kuchukua ngawira, tuacheni


tukufuateni! Wanataka kuyabadili maneno ya Allaah. Sema: Hamtotufuata kabisa.
Allaah Alikwishasema kama hivi zamani. Hapo watasema: Bali nyinyi
mnatuhusudu. Sio, bali walikuwa hawafahamu ila kidogo. [Al-Fat-h 48: 15].
Wale watu waliokuwa hai zama za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu alayhi wa
sallam) ndio wanaokumbushwa (wanaohusishwa na) Ayaah hizi kwa sababu ya
kutomtii. Baadhi yao walikuwa bado hai wakati wa Abu Bakr, Umar na
`Uthmaan (Radhiya Allaahu anhum), na kutii kwao wangelipwa ujira, na kuacha
kutii kwao ni adhabu kali. Huu ni unadi wetu kuhusu ukhalifa wao (Allaah
Awawie radhi wote) Na Allaah Asijaalie katika nyoyo zetu chuki dhidi ya mmoja
katika wao; kama moja ya ukhalifa wao ni imara, hivyo umethibiti ukhalifa wa
mmoja wao basi umekwenda kwa mpangilio ukhalifa wa wote wanne.

Swalah Ya Ijumaa Nyuma Ya Kila Imaam Muislamu, Sawa Wakiwa Wema Au


Waovu
Wanaonelea kuswali - Swalah ya Ijumaa na nyinginezo - nyuma ya kila Imaam
Muislamu, sawa akiwa ni mchaji Allaah au muovu. Hakika Allaah (Subhaanahu
wa Taala) Kaamrisha kuswali Swalah ya Jumuah kama wajibu kamili, pamoja na
elimu Yake Allaah (Taala) Anajua baadhi ya viongozi ambao wataojitokeza
watakuja kuwa mafajiri na mafasiqi. Hata hivyo hakutenga wakati na kuacha
wakati mwengine, wala hakuamrisha (utoaji wa) adhaana siku ya Ijumaa pekee
bila siku zingine.

27
www.alhidaaya.com

Jihaad Pamoja Na Viongozi Hata Kama Waovu


Wanaonelea kuwa kwa Jihaad dhidi ya Makafiri pamoja na Viongozi hata kama
watakuwa waovu, na wanaonelea kuwaombea duaa kwa wema na kurudi
kwenye uongofu. Na hawaonelei (kujuzu) kufanya Khuruuj (uasi) dhidi yao
(Viongozi) kwa kuwasimamishia panga wala mapigano kwa sababu ya
fitnah. Wanaonelea kujuzu kupigana pamoja na kiongozi muadilifu dhidi ya
makundi maovu ikiwa masharti ya hilo yatatimia.

Nchi Ya Kiislamu

Wanaonelea ya kwamba nchi ya Kiislamu si nchi ya kikafiri kama waonavyo


Mu`tazilah, maadamu tu wanaadhini (wazi) kwa ajili ya Swalah na utawala uko
wazi [wa Uislamu] na watu wake wanaweza kuitekeleza (Swalah hiyo) kwa
amani.

Matendo Ya Waja Hayawajibishi Kuingia Peponi, Bali Ni Kutokana Na Fadhila


Za Allaah

Wanaonelea ya kwamba mtu hawajibiki kuingia Peponi kutokana na matendo


yake - bila kujali hata akifanya matendo gani - ila ni kwa fadhila na rahma za
Allaah ambazo Huzihusisha kwa Amtakaye. Hata kama Allaah Asingelitoa
fadhila Zake, hakuna yeyote angeliweza kumwambia lolote. Kama Alivyosema
Allaah:

28
www.alhidaaya.com







Na lau kuwa si fadhila ya Allaah na rahma Yake juu yenu, asingelitakasika
miongoni mwenu kabisa hata mmoja. Lakini Allaah Humtakasa Amtakaye. [AnNuwr 24: 21].

Pia Kasema:







Na lau kuwa si fadhila ya Allaah juu yenu na rahma Yake mngelimfuata
shaytwaan ila wachache wenu tu. [An-Nuwr 4: 83].

Pia Kasema:

Na Allaah Humkusudia kumpa rahma Yake Ampendaye. [Al-Baqarah 2: 105].

Allaah Ndiye Ar-Razzaaq (Mwenye Kuruzuku Daima)

Na hakika Allaah (Taala) Humpa riziki, nguvu na chakula kila kiumbe hai katika
maisha yake. Naye Allaah ndiye Huvilisha viumbe waliosalia (wanyama n.k). Na
29
www.alhidaaya.com

ni Yeye ndiye Huruzuku katika (kutoa) Halali au Haramu. Hali kadhalika ni Yeye
ndiye Huruzuku mazuri na yanayotumika katika kupata hayo.

Allaah Ndiye Kaumba Mashayatwiyn Na Wasiwasi Wao


Wanaamini kwamba Allaah (Taala) ndiye kaumba shayaatwiyn wawatiao
wasiwasi watoto wa Aadam, kuwashawishi, kuwadanganya na kwamba
shaytwaan humuathiri binaadamu.

Uchawi Na wachawi

Kwamba katika dunia kuna wachawi na uchawi; na kwamba kuutumia uchawi ni


Kufr (ukafiri) na kuamini kwamba ndio unaoleta faida na madhara bila idhini ya
Allaah (Azza wa Jalla).

Kujitenga Na Bidah
Wanaonelea kujitenga mbali na Bid ah, pamoja na madhambi, kiburi, majivuno,
ulaghai, hila, rushwa na dhulma. Na wanaonelea (mtu) kuacha kabisa kuleta
madhara kwa watu na kuacha ghiybah (usengenyaji), isipokuwa kwa yule
anayeifanya na kuilingania Bidah hadharani, kumuongelea mtu huyo si
usengenyaji kwao.

30
www.alhidaaya.com

Kujifunza Elimu

Wanaonelea kwamba elimu ni lazima ichukuliwe (ya dini) na itafutwe kutoka


kwa watu wake. Na ichukuliwe mkazo sana katika kujifunza Qur-aan na sayansi
yake na tafsiri yake. Na kusikiliza Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa
sallam), kuzikusanya zote na kuzifahamu kwa yale yaliyomo; na kutafuta Aathaar
za Maswahaba.

Kujizuia [Kuwaongelea Vibaya] Maswahaba


Wanajiepusha kuwaongelea vibaya Maswahaba na kuwaeleza kiubaya
wao. Wanamkabidhi Allaah (Azza wa Jalla) kwa yale yaliyotokea baina yao.

Kushikamana Na Jamaaah

(Wananasihi watu wote) Kushikamana na Jamaaah. Wanakula, kunywa na kuvaa


kati kwa kati. Wanashaji`ishana kufanya kheri, kuamrisha mema na kukataza
maovu. Na kujiepusha na wajinga mpaka watapojua na kubainishiwa haki.
Halafu baada ya kubainishiwa haki wakaikataa, hapo udhuru utakuwa
umetoweka baina yao (waliyoikataa) na wao.

Uwajibu Wa Kushikamana Na Madh-hab Ya Ahlul-Hadiyth, Firqatun-Naajiyah


(Kipote Kitakachookoka)

31
www.alhidaaya.com

Huu ndio msingi wa Dini na Madh-hab, (hii ndo) itikadi ya Maimaam wa


Hadiyth ambao hawakuathiriwa na Bidah na wala hawakutumbukia katika
mambo ya fitnah. Wao si walaini katika masuala ambayo ni makruhu (yenye
kuchukiza) katika Dini, na wala hawatofautiani katika hili.
Na jua ya kwamba Allaah (Taala) Kawajibisha katika kitabu Chake mapenzi na
msamaha Wake kwa wale wataomfuata Mtume Wake (Swalla Allaahu alayhi wa
sallam) na Akawajaalia kuwa ni kikundi kitakachookoka (Firqatun-Naajiyah) na
kikundi kimfuatacho (Yeye). Kasema (Allaah) kumwambia anayedai kumpenda
Allaah (Subhaanahu wa Taala):

Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Allaah basi nifuateni mimi,


Atakupendeni na Atakufutieni madhambi yenu. [Al-`Imraan 03 : 31]

Allaah

Allaah Atujaalie sisi na nyinyi elimu na kuwa na taqwa (uchaji Allaah) kutokana
na shub-hah na upotofu kwa neema na rahma Zake.

32
www.alhidaaya.com

Anda mungkin juga menyukai