YALIYOMO
SURA YA KWANZA Baleghe..............................................................................................2 SURA YA PILI Mahusiano kati ya alama za kubaleghe na suala la hedhi................4 Jinsi Mwanamke atakavyo tambua kanuni za damu ya Istihadha...15 Yaliyoharamishwa kwa mwenye Janaba.........................................23 Mambo yaliyo karaha kwa mwenye Janaba................................... 24 SURA YA TATU Majosho ya Sunna...........................................................................34 SURA YA NNE Namna ya kuoga..............................................................................40 SURA YA TANO Masala mbali mbali ya akina Dada na Wanawake.........................42 Kuficha mapambo kutokana na asiye maharimu............................43 Mazungumzo kati ya mwanamke na asiyekuwa maharimu...........44 Wanawake kutazama filamu za michezo........................................50 Mwanamke kuhudumiwa na Tabibu Mwanamume.........................51 Jedwali ya Maasumina kumi na wanne...........................................52
NENO LA MCHAPISHAJI
Kitabu hiki kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Fiqhu l-Fatayaat kilichoandikwa na Mustafa Ranjbar wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran . Kitabu hiki chenye manufaa sana kinahudumia mahitaji ya wajibu wa dini ya Kiislamu ya mwanamke kuhusiana na vipindi vyake vya kila mwezi. Baadhi ya masala na hukumu za kuhudumia maiti ni makala muhimu zilizoongezwa kwenye kitabu hiki. Sharia na kanuni zilizowekwa na Uislamu kwa ajili ya namna ya maisha ya usafi iliyodhibitiwa ni wajibu kwa kila Mwislamu kujifunza na kuzipandikiza ndani ya nafsi yake. Hili ni dhahiri kabisa kwamba litamwezesha yeye kudumu ndani ya mipaka ya mahitaji ya kisharia yaliyowekwa. Shukrani zetu nyingi zimwendee ndugu yetu Ukhti Maysara Ali kwa kazi yake ya kutarjumi kitabu hiki. Vilevile shukrani zetu kwa wale wote waliochangia kwa njia moja au nyingine kwenye kufanikisha kukamilika kwa kazi hii tukufu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es- Salaam , Tanzania .
Kwa Jina la Mwenyeezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu SHARIA ZINAZO WAHUSU WATOTO WA KIKE
UTANGULIZI:
Ni jambo la wajibu juu ya (kila) mtu kujifunza masala ambayo yanamtokea mara kwa mara. (Hii ni kauli ya Wanavyuoni Ndani ya Vitabu vinavyohusu Matendo ya Kisharia.) Hakika kipindi cha ujana kinahesabika kuwa ndiyo fursa yenye thamani katika kujipatia maarifa na kuyavuta kutoka kwenye vyanzo vya elimu ambavyo mtu atafaidika navyo muda wote wa uhai wake. Kila umri wa mwanadamu unavyosonga mbele, ndivyo majukumu yake yanavyozidi na maisha yake kuwa na msongamano. Kwa hali hiyo basi hukosa fursa ya faragha itakayomruhusu kujifunza yale yanayomlazimu miongoni mwa kanuni za sharia, na maoni ya wanachuoni wa sharia, ambazo nyingi miongoni mwa hizo huenda atazihitajia katika maisha yake hapo baadaye. Bila shaka mwanadamu anahitaji kuwa na wigo katika kufanya mabadiliko ya kibinadamu ndani ya safari yake ya maisha. Na wigo huu ni mambo matatu yafuatayo:Kwanza: Utashi. Pili: Maarifa, na tatu: Ni Uwezo wa kusubiri na kuyavumilia matatizo mpaka afikie kwenye lengo. Kwa hali hiyo basi, mtu mwenye (tabia ya kuwa na) matarajio (bila kujituma) hawezi kuyafikia baadhi ya matarajio yake au yote, isipokuwa tu kama atakuwa amebeba ndani ya moyo wake utashi na mapenzi ya dhati katika kuiendea njia hiyo. Inampasa (mtu huyu) ajiandae kwa silaha ya maarifa na ujuzi utakaomnufaisha katika hilo, na awe na uwezo wa kusimama kidete kukabiliana na vikwazo na matatizo.
Na zaidi ya hayo yote ni kuwa; mwenye kupita njia ya haki na mwenye kutafuta wema wa dunia na akhera, anahitaji huruma na msaada wa Mwenyezi Mungu. Kadhalika (anahitaji kupata) uangalizi na usaidizi kutoka kwa Imamu wa zama hizi (Imamul- Mahdi a.s.) ili aweze kuendelea, na kuimarika juu ya njia ya uongofu wa Mwenyezi Mungu mpaka mwisho wa njia. Tumeandika mafunzo haya ambayo yanahusu kanuni za wanawake, ili nasi tupate kutoa mchango (wetu) miongoni mwa wale wenye mapenzi ya kuchukua maarifa (ya dini) kutoka kwenye chem chem asilia ya mafunzo ya sharia kutoka kwa kizazi cha watu wa nyumba ya Mtume s.a.w. Kisha juu ya hayo yameongezwa masala na uchambuzi mwingine, ambapo yamefikia hapo yalipo sasa. Wakati tunapo kiwasilisha kitabu hiki mbele ya dada zetu waumini (wa kawaida) na wale wahubiri wa kike wenye kufuata nyayo za Bibi Fatmah Zahraa (a.s) na bibi Zainab, tunataraji mtatupa maoni na rai zitakazo tunufaisha ili tuweze kuzitumia kwenye chapa zitakazofuatia Kipindi hiki tulicho nacho, ni kipindi cha kumbukumbu ya miaka kumi na minane tangu kuondoka kwa mmoja miongoni mwa waalimu wakubwa wa sharia ya ki-Islamu na muasisi wa jamuhuri ya ki-Isilamu ya Iran iliyobarikiwa, naye ni Imam Khomein (Mwenyeezi Mungu amrehemu). Tunamwomba Mwenyeezi Mungu Mtukufu Atuongoze katika yale Ayapendayo. Na (tunamuomba) ayakubali na kuyaridhia matendo yetu (mema). Na (tunamuomba pia) aturuzuku maombezi ya Mtume Muhammad (s.a.w.), na kizazi chake kilichotakasika. Na mwisho wa maombi yetu tunasema: Kila sifa njema ni ya Mwenyeezi Mungu Mola Mlezi wa Viumbe. Mustafa Ranjbar Shirazi. E- mail: Ranjbar85@yahoo.com
SURA YA KWANZA
Baleghe
Mwanzoni mwa kipindi cha ujana hutokea mabadiliko makubwa na ya kina ambapo nguvu za kimwili na kiroho hufunguka. Si hivyo tu, bali katika kipindi hichi ndani ya akili ya mwanadamu huchomoza matarajio na fikra mpya na kumwonesha kuwa anayo hadhi inayowavutia wengine kushirikiana naye. Bila shaka kuanzia hapo mtu huyu hukataa kuwa (mwenye) kufuata tu, ambapo sasa hutafuta uhuru katika mambo yake binafsi na katika maamuzi yake anayoyachukua. Hali hiyo humaanisha kuwa amefikia kipindi cha Baleghe na kuwa anataka kuchagua njia moja baina ya njia nyingi mbali mbali. Na njia hii (anayoitafuta) ni ile itakayo mfikisha kwenye wema wake binafsi, kama ambavyo ni wajibu wake binafsi kuichagua njia hiyo, kwani katika bahari hii yenye wingi wa fikra zinazo gongana huenda akajikuta anamhitajia (mwanachuoni) atakayemsaidia kumuongoza na kumvusha Swalama na kumfikisha ufukweni kwa amani. Basi ndani ya kipindi hiki, huruma ya Mwenyeezi Mungu humfunika na rehema humteremkia kwa msaada wa ujumbe unaokunjukiwa na muono unaotokana na aina (mbali mbali) za fikra, kwa lengo la kuzingatiwa misingi yake na kusomwa maandiko yake. Kwa hali hii basi, mara atajikuta anahisi furaha na kuingia katika mazingira mazuri hali ya kuwa uso wake ni wenye nuru na huku ulimi wake ukimhimidi na kumshukuru (Mola) juu ya yale aliyoelezwa na kule kufikia
2
1 -Mwaka Mwandamo ni Mwaka upatikanao kutokana na mzunguko wa Mwezi Mwandamo. (Mfasiri) 2 - Mwaka Mawiyo ni Mwaka wa kawaida uliozoeleka ujulikanao kama Mwaka wa Kizungu. (Mfasiri)
SURA YA PILI
Mahusiano kati ya alama za kubaleghe na suala la hedhi
Mara nyingi upatikanaji wa damu ya mwezi kwa wasichana hutokea kati ya umri wa miaka kumi na mbili hadi miaka kumi na nne. Tofauti hii inatokana na sababu za kimazingira, kijografia na kinasaba. Hivyo katika nchi zenye baridi damu ya mwezi huchelewa kuonekana mpaka kwenye umri wa kati ya miaka kumi na sita hadi kumi na nane. Na katika nchi zenye joto huonekana mapema kwenye umri wa kati ya miaka kumi hadi kumi na mbili. Msichana anapotimiza miaka tisa ya mwandamo analazimika kumrejea mwanachuoni mwenye daraja ya ijtihad aliyetimiza masharti. Atamrejea mwanachuoni huyo ili amfuate katika nadharia zake na rai zake zinazohusu sharia katika namna ya utekelezaji wa wajibu wa kisharia, kuanzia Swala, swaumu na sharia nyinginezo. Bila shaka vigawanyo vya damu ambayo huiona mwanamke ni vigawanyo saba, na kila kimoja kati ya hivyo kina kanuni zake mbalimbali za kisharia. Sisi tutavitaja vigawanyo hivi na kisha baada ya hapo tutazifafanua kanuni za wajibu.
4
6 -Somo la Damu ya Istihadha litakufikia muda mfupi ujao. 7 - Mwaka wa mawiyo ni mwaka uliozoeleka na unaojulikana kama mwaka wa kizungu. (Mtarjuma) 7
Masala:
Ni upi wajibu alionao mwanamke anapokuwa ndani ya siku za kujichunguza? Ni lazima kwa mwanamke ambaye ametimiza alama na masharti ya hedhi ajichunguze mwenyewe kwa muda wa siku tatu kuanzia pale linapotoka tone la kwanza la damu. Nini maana ya mwanamke kujichunguza kwa muda wa siku tatu? Jibu: Maana yake ni kuwa: Baada tu ya mwanamke kuona tone la kwanza la damu anatakiwa kuyaacha matendo yake ya kiibada kwa muda wa siku tatu mpaka itakapobainika hali yake upande wa wajibu wa kisharia na kujua je, atatumia kanuni za hedhi au atatumia kanuni za damu ya Istihadha? Kwa hiyo ndani ya siku hizi tatu, ni lazima kwake kuyaacha mambo yote yaliyoharamishwa kwa mwanamke mwenye hedhi. Na iwapo damu itaendelea kwa muda wa siku tatu bila kukatika atachukulia kuwa ni hedhi, na hapo atalazimika kutumia kanuni za hedhi. (Mfano, ikiwa siku hizi zimo ndani ya mfungo mtukufu wa Ramadhan ni lazima kwake kulipa swaumu na wala si lazima kulipa Swala.)
10
a. Ikiwa kutokana na sifa za damu anaweza kugundua ni ipi damu ya hedhi, na ni ipi damu ya Istihadha, basi analazimika kutenda kulingana na hali hiyo. b. Na ikiwa hawezi kutenganisha sifa za damu basi atarejea kwa jamaa zake ambao ni (Mama, dada na mama mdogo). Kwa hiyo atatambua siku za ada yake kwa kufuata ada zao. c. Ikiwa siku za hedhi kwa ndugu zake hazina ada maalumu, basi siku saba za mwanzo atazifanya kuwa ni hedhi, na siku zilizobaki atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha. Asiye na Ada Maalum: Iwapo ndani ya mwezi huu itatokea kuona damu zaidi ya siku kumi, basi atafuatilia sifa za damu. Endapo zinafanana na sifa ya hedhi, basi siku kumi za mwanzo atazifanya kuwa ni hedhi na zilizobakia atazifanya kuwa ni damu ya Istihadha. Na kama hazifanani na sifa ya hedhi, basi ni wajibu juu yake atende kulingana na vipengele viwili vya A na B vinavyohusu kanuni ya Mwenye Ada ya Wakati. Aliyesahau: Iwapo ataona damu zaidi ya siku kumi, basi anawajibika kutenda kulingana na hukumu za kifungu cha tano, yaani cha yule Asiye na Ada Maalum.
12
14
17
Alama
Wastani Nyingi Damu ilowanishe Damu itembee ichafue pande zote kutoka kwenye mbili za pamba bila pamba mpaka kutoka nje nje(kiasi cha ku tapakaa kwenye pendi au kitambaa)
Hukumu ya Swala
Kila Swala: 1. Kubadili pamba Pamoja na kutenda Pamoja na wajibu au pendi 2. Kutia Udhu 3. Kutoharisha mavazi na mwili sehemu iliyona jisika moja mambo matatu wa kutenda mambo yenye kushirikiana, matatuyenye kushi pia anawajibika kuo rikiana pia: ga kila siku mara 1. Kuoga kabla ya Swala ya asubuhi 2.Kuoga kabla ya Swala ya adhuhuri na alasiri(kwa shar ti iwapo atazikusa nya pamoja) 3.Kuoga kabla ya magharibi na isha (kwa sharti iwapo atazikusanya pamoja)
Hukumu ya Swaumu.
Sahihi wala haihi Sahihi kwa sharti Sahihi kwa sharti taji udhu ya kuoga josho la ya kuoga majosho la wajibu la kila ya wajibu ya kila siku siku.
18
19
20
Nne: Josho la Janaba: Mwenyezi Mungu amesema: Na mkiwa na janaba, basi ogeni10 Janaba ni nini? 1. Janaba hupatikana kwa mwanadamu kwa moja kati ya mambo mawili: 2. Kujamiana.
10 -Al-Maida: 6. 21
22
23
Nukta Muhimu:
Iwapo mtu atapatwa na janaba kisha akaoga, basi kuanzia hapo si karaha kwake kutenda mambo yaliyotajwa hapo juu.
24
2. Kuinyoosha mikono yake kwenye mbavu zake, kunyoosha miguu yake na kumfunika kwa nguo. 3. Kumuwashia taa usiku. 4. Kuwaarifu waumini ili wahudhurie mazishi yake. 5. Kuharakisha kumuandaa (isipokuwa kama kuna utata wa hali yake, hivyo atasubiriwa mpaka upatikane uhakika wa kifo chake). 6. Atakapofariki mjamzito, basi ni wajibu kumtoa mtoto tumboni (akiwa yuko hai) na ndipo azikwe.
29
30
(VII) Mazishi:
Baada ya kumwosha ni lazima kumpaka karafuu maiti kisha kumvisha sanda, halafu kumswalia na hatimaye mwili kuzikwa ardhini kwa namna ambayo itazuia harufu kutoka nje, au kufukuliwa na wanyama.
Nukta Muhimu:
Ndani ya vitabu vya dua na vitabu vya matendo ya kisharia vya waheshimiwa wanachuoni wetu wakuu, kumepatikana mafunzo na sunna nyingi zinazohusiana na mazishi. Miongoni mwa vitabu hivyo, ni kitabu kiitwacho Mafatihul-Jinani cha Sheikh Abasi Al-Qummi. Kwa mwenye kutaka ziyada arejee humo.
32
33
SURA YA TATU
Majosho ya Sunna
i. Majosho ya Sunna ya wakati maalum. ii. Majosho ya Sunna ya sehemu maalum. iii.Majosho ya Sunna kwa ajili ya vitendo maalum
2. Siku zote za usiku tasa unaopati kana ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadha
3. Usiku wa 15,17,19,21,23,25,27,na Kati ya Magharibi na Isha 29 katika mwezi mtukufu wa Ramadhani (ni Sunna iliyohimi zwa) 4. Usiku wa ishirini na tatu ya mwezi Mwisho wa usiku wa Ramadhan (josho la pili) 5. Siku ya siku kuu ya Idi ya Kuanzia kuchomoza kwa alfajiri kufungua (ni Sunna iliyohimizwa) mpaka adhuhuri, na huenda ikawa ni mpaka kuzama kwa jua.
34
6.
Siku kuu ya Idi ya Kuchinja (ni Sunna iliyohimizwa) Siku ya nane ya Mfungo tatu (Siku ya Tar'wiya) Siku ya tisa ya Mfungo tatu (Siku ya Arafa) (Mwezi wa Rajabu) Siku ya kwanza ya Mfungo kumi, ya mwisho na nusu yake Siku ya Maapizano Mubahala (Mwezi ishirini na nne ya Mfungo tatu) Siku ya Maapizano Mubahala (Mwezi ishirini na nne ya Mfungo tatu) Mfungo pili
Kuanzia kuchomoza kwa alfajiri mpaka adhuhuri, na inaweze kana mpaka kuzama kwa jua Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi Wakati wa Adhuhuri ni bora zaidi
7. 8. 9.
10.
11.
35
Wakati
3.
shoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake. 4. Josho kwa ajili ya kuingia kaaba Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunato sheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake Kuoga mwanzo mwa mchana kunatosheleza kwa ajili ya kuingi a mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
5.
36
Josho kwa ajili ya kuingia Madina Kuoga mwanzo mwa mchana kuna Yenye Nuru tosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwa nzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake
7. Josho kwa ajili ya kuzuru Msikiti Kuoga mwanzo mwa mchana kuna wa Mtume tosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake. 8. Josho kwa ajili ya kuzuru maeneo Kuoga mwanzo mwa mchana ya makaburi matukufu ya kunatosheleza kwa ajili ya kuingia Maimamu Waliyo takaswa mwishoni mwake, na kuoga mwanzo wa usiku kunatosheleza kwa ajili ya kuingia mwishoni mwake.
37
Wakati
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku
2.
3.
4.
5.
Josho kwa ajili ya Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo kusimama Mash'ari mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kutenda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku.
38
6.
Josho kwa ajili ya kuchinja Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. na hivyo hivyo kwa upande wa usiku. Josho kwa ajili ya kunyoa nywele (Hija) Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. na hivyo hivyo kwa upande wa usiku.
7.
8.
Josho kwa ajili ya kumwona Kabla ya kitendo, na si vibaya Ma'suum (a.s.) usingizini kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku. Josho kwa ajili ya Swala ya Kabla ya kitendo, na si vibaya Haja kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku. Josho kwa ajili ya Istikhara Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa Usiku.
39
9.
10.
Kabla ya kitendo, na si vibaya kuwepo mwanya kati ya kuoga mwanzoni mwa mchana na kute nda mwishoni mwake. Na hivyo hivyo kwa upande wa usiku. Kabla ya kitendo Kabla ya kitendo Kabla ya kitendo
12.
13. Josho la kumzuru Imamu Husein (a.s.) 14. Josho la Swala ya Kuomba mvua
SURA YA NNE
Namna ya kuoga
Majosho yaliyotangulia kutajwa hapo kabla, unaweza kuyatimiza kwa namna moja kati ya namna mbili: Utaratibu Maalum: Niya: Kisha kuosha kichwa na shingo. Kuosha upande wa kulia wa mwili pamoja na tupu mbili. Kuosha upande wa kushoto wa mwili pamoja na tupu mbili.
40
SURA YA TANO
Masala mbalimbali ya akina Dada na Wanawake
Je ni wajibu mwanamke kujisitiri uso wake kutokana na wanaume wasiyo muhusu kwa mujibu wa Sharia? Swali: Iwapo Mwanamke atatambua kuwa mwanaume asiye maharimu wake anautazama uso na viganja vyake kwa matamanio, je ni wajibu juu ya mwanamke huyo kujisitiri uso na viganja?
11 -Kuna tofauti kati ya Wanazuoni wa Sharia juu ya suala hili, hivyo Muqalidi arejee kwenye rai ya Mujtahid wake. 12 - Kuna tofauti kati ya Wanazuoni wa Sharia juu ya suala hili, hivyo Muqalidi arejee kwenye rai ya Mujtahid wake. 42
43
44
Swali:
Ni ipi tofauti iliyopo kati ya wimbo na muziki, na ni ipi hukumu yake?
13 -Al-Biharu, juz 103. 45
46
Swali:
Ni ipi hukumu ya kusikiliza muziki ambao unarushwa na idhaa na Runinga (katika Jamuhiri ya ki-Islamu) au mamlaka ya ki-Isilamu. Ni ni ipi hukumu ya kutengeneza, kujifunza, kuuza na kununua vyombo vya muziki?
Jibu:
1. Samahatu Ayatullah Sistani:Ikiwa muziki hauna uhusiano na maeneo ya upuuzi na uharibifu basi si vibaya. 2. Samahatu Ayatullah Khamenei: Kila aina ya sauti zinazo pumbaza, za upuuzi zijulikanazo kwenye maeneo ya ufasiki na uovu ni haramu. Kuuza na kununua vyombo vinavyotumika ni haramu na hairuhusiwi. Ama kuhusu vipindi vya idhaa na Runinga ili kuainisha maudhui husika kunategemea mtazamaji na msikilizaji. Hivyo akiamini kuwa muziki huu ni wenye kupumbaza na upuuzi au kipindi hiki hupelekea uharibifu, basi ni lazima kutokusikiliza na kutokutazama, (na kwa ujumla ni kuwa, kurusha muziki kunapingana na malengo mema ya utawala wa ki-Islamu). 3. Samahatu Ayatullah Lan-Karani: Ikiwa muziki unapumbaza na una amsha hisia, na ni mashuhuri kwa watu waovu, basi muziki huo utakuwa haramu, na usiyokuwa na sura hii hauna kizuizi, na wala upande unaoutangaza hauathiri hukumu.
47
Kucheza
1. Samahatu Ayatullah Khomeni: Kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu ni kwamba hairuhusiwi kwa wanawake kucheza sehemu yoyote ile, mfano kwenye hafla ya ndoa, harusini au kwenye mashairi (isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe). 2. Samahatu Ayatullah Khamenei: Kwa ujumla kucheza kuna utata isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe mbali na macho ya wengine. 3. Samahatu Ayatullah Bahjati: Kucheza kwa namna yoyote ile kuna utata. 4. Samahatu Ayatullah Makarimu Ash-Shirazi: Isipokuwa kucheza kwa mwanamke kwa ajili ya mumewe tu ndiko kunaruhusiwa. Ama kulikobaki kuna utata. 5. Samahatu Ayatullah Sistani: Kwa mujibu wa ihtiyati ya wajibu hairuhusiwi, isipokuwa mwanamke kucheza kwa ajili ya mumewe mahali ambapo hakuna mtu mwingine yeyote. 6. Samahatu Ayatullah At-Tabrizi: Kucheza ni katika mambo ya upuuzi, na hakumfai muumini.
49
50
51
Tarehe ya kufariki
Mwezi 28 Swafar (Mfungo tano) mwakawa 11 Hijiriyyah
Alikozikwa
Madina;Saudi Arabia.
Imam Ali bin Abi Mwezi 13 Rajab Mwezi 21 Rama Talib a.s. Mwaka wa 23 dhan mwaka wa kabla ya Hijrah 40 Hijiriyyah. Fatimah binti Muhammad a.s.
Najaf; Iraq.
Mwezi 20 Jamadil Mwezi 3 Jamadil- Madina; Saudi Akhar (Mfungo Akhar (Mfungo Arabia. tisa) Mwaka wa 8 tisa) mwaka wa 11
kabla ya Hijrah
Imam Hasan bin Ali a.s. Mwezi 15 Ramadhani, Mwezi 28 Swafar (Mfungo tano) Madina;Saudi Arabia.
mwaka wa 3 Hijiriyyah
Imam Husein bin Ali a.s.
mwaka wa 50
riyyah
mwaka wa 61 Hijiriyyah
52
Mwezi 5 Shaaban Mwezi 25 Muharram Madina mwaka wa 38 Hiji (Mfungo nne) mwaka Saudia Arabia
riyyah Imam Muhammad bin Ali a.s. Mwezi 1 Rajab mwaka wa 57 Hijiriyyah
wa 95 H Mwezi 7 Dhul-hijja Madina; (Mfungo tatu) Saudi Arabia mwaka wa 114 Hijiriyyah
Madina; Saudi Arabia
Imam Ja'far bin Mwezi 17 Rabiul- Mwezi 25 Shawwal Muhammad a.s. awwal (Mfungo (Mfungo mosi)
Hijiriyyah
Khurasaan; Iran
53
Imam Ali bin Mwezi 2 RabilMwezi 3 Rabiul Samarraa Muhammad a.s. Akhar (Mfungo saba) awwal (Mfungo Sita) Iraq
Imam Hasan Mwezi 8 Rabil-Akhar Mwezi 8 Rabiul-awwal Samarra; bin Ali a.s (Mfungo saba) mwaka (Mfungo Sita) mwaka Iraq
wa 260 Hijiriyyah
Mwezi 15 Shaaban Bado yu hai na yuko mwaka wa 255 katika Ghaiba kuu. Hijiriyyah
54
58
Ni jambo la wajibu juu ya kila mtu kujifunza masala ambayo yanamtokea mara kwa mara.Hii ni kauli ya wanavyuoni wa kifikihi iliyodondolewa kutoka vitabu vya fatwa au hukumu za kifikihi. Hakika kipindi cha ujana kinahesabika kuwa ndiyo fursa yenye thamani katika kujipatia maarifa na kuyavuta kutoka kwenye vyanzo vya elimu ambavyo mtu atafaidika navyo muda wote wa uhai wake. Kila umri wa mwanadamu unavyosonga mbele, ndivyo majukumu yake yanavyozidi na maisha yake kuwa na msongamano. Kwa hali hiyo, basi hukosa fursa ya faragha itakayomruhusu kujifunza yale yanayomlazimu miongoni mwa hukumu za sharia za Kiislamu, na maoni ya wanavyuoni wa sharia, ambazo nyingi miongoni mwa hizo huenda atazihitajia katika maisha yake hapo baadaye. Bila shaka mwanadamu anahitaji kuwa na wigo katika kufanya mabadiliko ya kibinadamu ndani ya safari yake ya maisha. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info
59