Anda di halaman 1dari 1

Maswali

1. Mwalimu umefundisha kuhusu upendo. Ninaomba unisaidie “kuna mtu ambaye kila ukiwa
karibu yake lazima uumie. Aidha kwa maneno au akufanyie kitu chochote ila mradi tu ukae
huna amani, na mtu huyo hata akijua amekukosea hawezi kukiri na kuomba msamaha;
lazima wewe uliyekosewa ukaombe msamaha.
a. Je, huyu mtu niishi naye vipi? Kwani ninapo kaa mbali naye nakaa kwa amani, lakini
nikiwa karibu naye lazima asababishe maumivu.
b. Mwalimu ni upendo upi naweza kumwonyesha huyu mtu akabadilika? Wakati
mwingine nakata tamaa naye.
2. Inanishangaza sana utaona mtumishi/watumishi wengine wanahubiri na kuhubiri lakini
hataki kusalimia mtu. Mtu huyu anamatatizo gani?
3. Kwa nini makanisa mengine hawapendi wanawake kuhubiri. Je, ni dhambi au desturi tu?
Mungu anaweza kuwahukumu kwa sababu tu walihubiri? Maana roho mtakatifu ametupa
wote wanaume na wanawake
4. Waefeso 4:26-27 – Kulingana na andiko hili, haipaswi jua lichwe na uchungu moyoni.
a. Je, andiko hili linamhusu nani?
b. Mbona kuna watu ambao wameokoka lakini wana hasira za miaka mingi?
Tusaidie tujue ni nani hasa anahusika na andiko hili kama ni:
Wachungaji, wainjilisti, maaskofu nk
5. Sabato ni nini? Na ni siku gani hasa?
6. Je, mtu akiokoka na kubatizwa kwa maji na roho, akarudi nyuma akakumbuka dhambi
aliyofanya akatubie? (Deliverance)
7. Deliverance – Kuvunja madhabahu za babu na bibi?
8. Umetufundisha kuwa kila sehemu (zamani) ina utamaduni wake. Je, sisi wakristo kanisani
(wanawake) ni nguo gani zinazotupasa kuvaa kwa utamaduni wetu wa kumpendeza Mungu?
9. Mungu anasema kwamba kusamehe ni vizuri na ukisamehe usiweke kinyongo chochote.
Lakini
a. Nimekusamehe lakini sitakusahau. Kwa nini Mungu yeye alimsamehe Musa lakini
hakumruhusu kuingia nchi ya ahadi? (Nimekusamehe lakini sitasahau)
10. Mathayo 4:1- Yesu alifunga siku arobaini kabla ya pasaka na wengine kama makanisa
wanafanya hivyo (sisi tunafunga kabla ya wengine, tena tunafunga pungufu),
a. Je, hatuendi kinyume na maandiko?
b. Au ni sheria ya wapentekoste?

Anda mungkin juga menyukai